Terms and Conditions

Masharti na Vigezo

Image

Kuhusu Kampuni

Smart Sports Tanzania Ltd ni kampuni iliyoanzishwa mwaka 2010, yenye ofisi Sinza Madukani, Dar es Salaam – Tanzania, inayojihusisha na uuzaji wa vifaa vya michezo pamoja na huduma ya uchapishaji wa jezi kwa kuweka majina, namba na nembo. Kampuni pia inatoa huduma ya usafirishaji wa bidhaa popote ulipo.

Matumizi ya Tovuti

Mtumiaji anakubali kutumia tovuti hii kwa madhumuni halali pekee. Hairuhusiwi kutumia tovuti kwa njia yoyote inayoweza kusababisha madhara, kuingilia usalama wa tovuti, au kukiuka sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bidhaa na Huduma

Bidhaa na huduma zote zinazoonyeshwa kwenye tovuti zinategemea upatikanaji. Smart Sports Tanzania Ltd tuna haki ya kubadilisha bei, maelezo ya bidhaa au kusitisha bidhaa au huduma yoyote bila taarifa ya awali.

Oda na Malipo

Kwa kufanya oda, mteja anakubali kutoa taarifa sahihi na kamili. Malipo yanapaswa kufanyika kulingana na maelekezo yaliyotolewa. Kampuni ina haki ya kukataa au kusitisha oda endapo kutakuwa na hitilafu, udanganyifu au ukiukwaji wa masharti haya.

Huduma ya Kuchapisha Jezi

Kwa bidhaa zinazochapishwa majina, namba au nembo, mteja anawajibika kuthibitisha usahihi wa taarifa kabla ya uzalishaji. Smart Sports Tanzania Ltd haitawajibika kwa makosa yatokanayo na taarifa zisizo sahihi zilizotolewa na mteja.

Usafirishaji

Tunatoa huduma ya usafirishaji ndani na nje ya nchi. Muda wa kufika kwa mzigo unaweza kutofautiana kulingana na eneo. Kampuni haitawajibika kwa ucheleweshaji unaosababishwa na wahudumu wa usafirishaji au sababu zisizo chini ya udhibiti wetu.

Marejesho na Mabadiliko

Bidhaa maalum zilizochapishwa kwa mahitaji ya mteja haziwezi kurejeshwa isipokuwa pale palipo na kasoro iliyosababishwa na kampuni. Masharti ya marejesho yataelezwa kwenye sera ya marejesho (Refund Policy).

Haki Miliki

Maudhui yote ya tovuti hii, ikiwemo maandishi, picha, nembo na miundo, ni mali ya Smart Sports Tanzania Ltd na hayaruhusiwi kunakiliwa au kutumiwa bila idhini ya maandishi.

Mabadiliko ya Masharti

Smart Sports Tanzania Ltd tuna haki ya kubadilisha masharti haya wakati wowote. Mabadiliko yote yataanza kutumika mara baada ya kuchapishwa kwenye tovuti.

Mawasiliano

Kwa maswali au maelezo zaidi kuhusu masharti haya, tafadhali wasiliana nasi kupitia tovuti au ofisi zetu. Au piga +255 715 995 111

Image NewsLetter
Newsletter

Subscribe our newsletter

By clicking the button, you are agreeing with our Term & Conditions

Your experience on this site will be improved by allowing cookies Cookie Policy